Sunday, May 12, 2013

"AKINA DADA ACHENI KUJICHUBUA....NJOONI NIWAPE MBEGU ZANGU ZA KIUME ZIWANG'ARISHE"....HII NI KAULI YA MBUGE KESSYY



MBUNGE wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy (CCM) alhamisi  ya  wiki  hii  aliwavunja mbavu wabunge baada ya kuwasuta wabunge wanaojichubua ngozi akiwaambia wanaohitaji ngozi nyeupe wamuone.



Ameitaka pia Serikali isiishie kukamata waingizaji wa vipodozi hatari, bali pia watumiaji wakiwemo wabunge. Kessy alisema Serikali inapaswa ikamate na watumiaji wa vipodozi hivyo kama ambavyo huwa inafanya kwa waingizaji na watumiaji wa dawa za kulevya.


Akichangia wakati wa kujadili vifungu kabla ya kupitisha bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii juzi, alisema inashangaza kuona katika meza za kujipodoa za wanawake wakiwemo wabunge, vimejaa vipodozi lakini serikali haiendi kuwakamata.


Alisema hata bungeni wapo wanawake wanaotumia dawa za kubadilisha sura kiasi kwamba wakienda vijijini kwao, ndugu zao wanawakimbia, lakini Serikali haiwakamati.



“Wanajiharibu sura huwezi kujua ni raia wa nchi gani; unashindwa kujua hawa ni Wachina, Wajapani ukianzia humu humu bungeni,” alisema Kessy na kusababisha kicheko bungeni.

Mbunge huyo aliendelea kuwavunja mbavu pale ambapo alisema wanaotaka kubadilisha rangi zao, wawaone watu weupe kama yeye wawape mbegu.


Kessy alitoa utani huo baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kumtania akisema “Na wewe ni matokeo ya vipodozi hivyo,” akimaanisha weupe wa Mbunge huyo.

“Nashauri wanaotaka kubadilisha rangi zao watuone sisi tuwape mbegu,” alisema na kuendelea kusababisha ukumbi mzima wa bunge ulipuke kwa kicheko.

Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi alisema jukumu la wizara yake ni kuangalia usalama wa vipodozi na haijihusishi kujua nani anatumia na nani hatumii.


Alisema wajibu wake ni kuhakikisha vipodozi vinavyoingia nchini vinakuwa na viwango. Alisema wanaotumia ni hiari yao kwa kuwa Wizara ikiingilia, utakuwa ni ubaguzi wa kijinsia.


Hata hivyo, Dk Mwinyi alisema watumiaji wanapaswa kuhakikisha kwamba vipodozi husika vimethibitishwa usalama wake.

No comments:

Post a Comment