Jumapili ya May 12 mwaka huu ni siku ambayo Lady Jay
Dee aliwaalika fans wake zaidi kuangalia kipindi cha ‘Diary ya Lady
JayDee’ kupitia EATV ili kufahamu kile alichokiita ‘uongo uliojificha’,
na kutoa mfano wa style ya Shaggy kukana na kusema ‘it Wasn’t me’, hata
kama ukinaswa na
Katika kipindi hicho cha jana jumapili (may 12) wameonekana wasanii wa
THT Linah na Barnaba ambao walieleza kuwa watakuwepo katika show ya
miaka 13 ya Lady Jay Dee kumsapoti, na kwa pamoja wasanii hao walitaja
kiingilio na kwamba watu wahudhurie ili kumsapoti Jide ambae ni dada yao
na mama yao mpendwa.
Lakini Barnaba na Linah hivi karibuni walikana kuwa hawatahudhuria
katika show ya Jide ya May 31 itakayofanyika Nyumbani Lounge licha ya
kuwa katika matangazo, na sababu ikiwa kutofikia maafikiano ya
kibiashara na uongozi wa wasanii hao. Na kwamba hakuna makubalino yeyote
yaliyofikiwa kati yao, lakini pia walisema hawana ugomvi na Lady Jay
Dee.
Kwa upande wa Jide yeye anasema alishalipia advance kwa ajili ya kufanya
kazi na wasanii hao wa THT na ndiyo sababu wako kwenye posters. Na
kwamba anajua watakuwa wamekatazwa na maboss wao.
Hapa kuna mkanganyiko wa maelezo na ni vigumu kufahamu nini kiko nyuma
ya pazia, makubaliano ya awali hadi kufikia hatua ya kushoot kipande
hicho cha tangazo. Na kwa nini wasanii hao wanakataa kata kata kuwa na
makubaliano na Jide kuhudhuria show yake.
Ni yapi maoni yako kuhusu hiki kinachoendelea?
No comments:
Post a Comment