Friday, May 10, 2013

ALIYEJIBADILISHA JINSIA NA KUWA MWANAMKE ATAKA BARAZA LA MTIHANI LISHURUTISHWE KUBADILI VYETI VYAKE NA KUWA NI MWANAMKE





BAADA YA KUJIBADILISHA
MWANAUME aliyegeuza jinsia yake, amelishtaki baraza la mitihani nchini, Kenya National Examination Council (KNEC), akitaka lishurutishwe kubadilisha vyeti vyake kuonyesha kwamba ni mwanamke.


Bi Audrey Mbugua ambaye awali alifahamika kwa jina la Andrew Ithibu kabla ya kubadilisha jinsia yake, anataka cheti chake cha mtihani wa kidato cha nne (KCSE) kionyeshe kwamba ni mwanamke.
Aliambia mahakama kwamba aligunduliwa kuwa na dosari ya jinsia 2001, na amekuwa akikabiliana na shida nyingi kwa sababu anatambuliwa kama mwanaume katika vyeti vyake.





Paul Wasanga
Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) Paul Wasanga.

“Nimejaribu kuomba KNEC mara nyingi ibadilishe jina langu katika cheti changu vya mtihani wa KCSE ili kionyeshe jinsia yangu halisi bila kufaulu,” Bi Audrey aliambia mahakama.
Alisema hatua ya KNEC kukataa kufanya mabadiliko hayo, imemsababishia mateso mengi kwa kubaguliwa na kunyimwa kazi. Mahakama ilimruhusu kuwasilisha ombi la kutaka baraza hilo liagizwe kutekeleza majukumu yake kwa kurekebisha jina lake liwe na mwanamke.
Siku 14
Anataka pia baraza hilo iagizwe kubadilisha alama inayoonyesha jinsia yake inayoonyesha ni mwanaume katika cheti hicho na badala yake ionyeshe kuwa ni mwanamke.
Mahakama ilipatia KNEC na Mkuu wa sheria muda wa siku 14 kujibu ombi la Bi Audrey.

Kesi itatajwa Mei 28 ili mahakama itoe maagizo zaidi.

No comments:

Post a Comment