Friday, May 10, 2013

Exclusive: Barnaba amshirikisha Kidum kwenye wimbo uliodhaminiwa na Barclays Bank – ala shavu la mil 25

Hitmaker wa Sorry, Barnaba amerekodi wimbo na msanii nguli wa Burundi aishiye nchini Kenya, Kidum uliofanyika jijini Nairobi, Kenya chini ya producer Kelly.
kidumu na barnaba
Wimbo huo uitwao Wamama umerekodiwa kwa udhamini wa benki ya Barclays ambayo ni miongoni mwa wadhamini wa kampeni ya Montage Charity Ball 2013’ iliyoanzishwa na Teddy Mapunda kwaajili ya kukusanya fedha kusaidia afya za wanawake.
Barnaba ameiambia Bongo5 kuwa gharama ya kurekodi wimbo huo pamoja na malipo yao, usafiri na malazi ni zaidi ya shilingi milioni 25.
Amesema moyo wake wa kujitolea katika masuala ya kijamii, ni sababu kubwa ya kuchaguliwa na kampuni ya Montage Limited kurekodi wimbo huo.
“Nimeamua kuimba kuhimiza watu kuchangia afya za akinamama kwasababu mama anapokuwa vizuri basi kizazi cha mama ama mtoto pia naye atakuwa vizuri,” amesema Barnaba.
Msikilize zaidi hapa.


“Unafahamu kabisa kwamba wamama wanakosa zahanati nyingi za kujifungulia, zahanati za kwenda kucheck clinic afya za watoto wao. Kwahiyo nikaamua kujitolea tu lakini mafanikio na vitu vilivyokuja au thamani ya kitu imekuja baada ya moyo wangu kujitolea na kukubali ndio Barclays wakaamua kusponsor safari yangu na kiasi cha fedha tulichopewa, kilikuwa na baada ya Barclays kuaminia kwamba Barnaba anaweza kufanya vizuri, ndio maana walinilipa vizuri.”

Sherehe za kuzindua mradi huo zitafanyika tarehe 8 mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment