Tuesday, May 7, 2013

HUYU NDIO MUIGIZAJI ANGA'NGANIA WATOTO WA MICHAEL JACKSON, HUU NDO USHAHIDI ALIOTOA




MUIGIZAJI nyota kutoka nchini Uingereza, Mark Lester amesema anaendelea na taratibu za kuthibitisha kuwa watoto wa Michael Jackson ni wake.
Nyota huyo amesema anaendelea na taratibu za kupima vinasaba (DNA) ili kuthibitisha kwamba Prince, Prince II, na Paris pia ni watoto wake.Hayo yalibainishwa katika gazeti la Mirror nchini Uingereza.
“Siwezi kufanya vipimo vya vinasaba kama sijapata kibali kutoka kwa watoto pindi watakapokuwa kiumri na si muda mrefu wataamua mimi kufanya hivyo, nami nitafanya," alisema Nyota huyo.

Lester, ambaye aling'ara katika wimbo wa Oliver alikuwa rafiki wa muda mrefu wa Michael Jackson kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Pia nyota huyo alisema, mwanadada Paris amefanana kwa kila kitu na binti yake, Olivia.

Tangu Lester aanze kutoa malalamiko yake hayo kwa mujibu wa Mirror, alisema familia ya Jackson imekata mawasiliano yote na yeye.

Kwa mujibu wa Mirror, Lester halizuiliwa kuwaona watoto tangu kifo cha Michael Jackson mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment