Thursday, May 9, 2013

HUYU NDIYE ANAYETARAJIWA KUWA MRITHI WA MIKOBA YA SIR ALEX FERGUSON PALE OLD TRAFFORD



Kuna taarifa kuwa mabingwa wa England, Manchester United wameanza mazungumzo na Kocha wa Everton, David Moyes.





Man United wanataka Moyes achukue nafasi ya Alex Ferguson ambaye ametangaza kustaafu mara baada ya msimu huu kwisha.




Ferguson ndiye kocha mwenye mafanikio zaidi England, ameamua kutundika daruga zake za ukocha na sasa Man United inaamini Moyes ndiye chaguo sahihi.


Inawezekana kama hawatawezakana, basi mazungumzo yatahamia kwa Jose Mourinho inagawa Man United inaonekana kuhofia tabia ya Mreno huyo ya kutopena katika timu moja.












Imeelezwa Ferguson aliwaeleza wachezaji wake kuhusiana na uamuzi wake wa kuachia ngazi mwishoni mwa msimu baada ya kuwaalika kuhudhuria mbio za farasi.

Ferguson aliwaalika wachezaji hao na walikuwa wametokelezea katika vazi la suti na mwisho akawaeleza uamuzi wake huo akionyesha hakuwa ametaka kuwashitua sana

No comments:

Post a Comment