Thursday, May 9, 2013

LADY JAYDEE KUWAUMBUA LINAH NA BARNABA, HII NDO NJIA ATAYOTUMIA

Kumekuwa na kupishana/vutanikuvute kati ya LadyJay Dee na wasanii wa THT Linah na Barnaba kuhusu wasanii hao kuwepo ama kutokuwepo kwenye show ya Jide May 31, hata hivyo Lina na Barnaba walithibitisha kuwa watakuwepo kwenye tamasha la miaka 13 ya Lady JayDee licha ya kuwa kwenye posters za show hiyo.



Leotainmenttz imeamua kufuatilia kiundani kupata maelezo ya pande mbili, kwa upande wa Barnaba na Linah wao walithibisha kupitia mtandao wa Bongo5 kuwa hawatahudhuria kwa sababu zifuatazo:

Linah: Dada yetu alituita akatuambia ana kazi yake ya kutimiza miaka 13 kwa hiyo anahitaji wasanii ambao watamsupport kwa ajili ya kufanya show. Sisi tulifuata protocol zote kwa sababu kama wasanii tuna viongozi, tukafuata protocol zote kuweza kukubaliana nae mpaka tukafikia hatua kwenye maswala ya biashara, yaani malipo. Kwenye upande huo kidogo tukawa tumepishana kwenye masuala ya maslahi. Lakini sasa tunashangaa yeye kuanza kuweka posters na nini. Yaani tumeshafikia makubaliano kwamba kulingana na maslahi haiwezekani.

Barnaba:
 Hatukushindwana, lakini unafahamu kila mwanasanaa, wale wote wanaofuata utaratibu wa sanaa wanakuwa wanamanejimenti zao na wanakuwa na matakwa ya ofisi zao. Kwa hiyo swala ni dadisi na ni refu na kazi limeletwa kwenye mdahalo…hata hivyo kulikuwa na booking ya kazi nyingine zilizokuwepo. Kwa hiyo mwisho wa siku imeonekana haitawezekana kwa sababu kuna kazi nyingine zimeshabukiwa. Tofauti zetu zilikuwa pale ambapo unaenda kuzungumza na mtu wakati hauna uhakika kama atakuwepo ama hayupo. Kwa hiyo hakuna tulichoshindwana bali ofisi/management ilikuwa na kazi tayari na makubaliano yetu yalikuwa hapo kwamba hatutoweza kuwepo kutokana na makubaliano ambayo yako kwenye ofisi na ofisi.”

Barnaba alisisitiza kuwa wao hawatakuwepo na kwamba hawana kabisa ogomvi na Lady JayDee na wanaongea vizuri tu.

Kwa upande wa Lady JayDee leotainmenttz imekuwa ikifuatilia tweets zake zinazoendana na kuwepo kwa Barnaba na Linah kwenye kipindi cha Diary ya LadyJayDee kinachorushwa na EATV. Na hii  ni baada ya TID kuwepo kwenye kipindi hicho wiki iliyopita na kuzungumzia kuwepo kwake kwenye show ya Miaka 13 ya Lady JayDee Nyumbani Lounge. 

Tweet za Jide kuanzia jumapili iliyopita zilisisitiza kuwa angekuwepo TID kwenye kipindi hicho, lakini kipindi cha jumapili hii kitakuwa kitamu zaidi kwa sababu atakuwepo Linah na Barnaba. Kama ni kweli watakuwepo, je wasanii hao wataelezea kuwepo katika show ya Jide kama alivyofanya TID? Tunapata mashaka kuwa inawezekana kutokana na tweet za Jide.

Tweet zake nyingine hazitaji majina ya wasanii hao lakini zinataja siku na kuonesha kuwa labda watakana hata wakionekana kwenye TV, akitoa mfano wa style ambayo aliitumia Shaggy kumshauri mwenzake Ricardo RikRok aliyefumaniwa katika wimbo kukana na kusema hakuwa yeye “It wasn’t me”, hata kama alinaswa kwenye camera.


Hizi ni baadhi ya Tweets za LadyJadee: 
Style ya Shaggy ya kushikwa mpk ktk camera na unasema wasn't me kiboko. Ndio kinachofuata
— Lady JayDee (@JideJaydee) May 4, 2013

Diary la leo tamu ila la wiki ijayo tamu zaidi. Barnaba na Linah ndani usikose usikose eeeh!!
— Lady JayDee (@JideJaydee) May 5, 2013

Diary ya Jd j'pili hii ijayo. Majibu ya uongo ulofichwa. Naupenda kweli wimbo wa Shaggy It wasn't me, sijui nini nini on camera It wasn't me
— Lady JayDee (@JideJaydee) May 8, 2013

She saw me banging on a sofa. It wasn't me. She even caught me on camera.It wasn't me OMG. OMG OMG
— Lady JayDee (@JideJaydee) May 8, 2013
Kwa kuwa ni kitu cha kuonekana kwenye TV tusubiri tushuhudie nini kitaonekana kwenye Dairy ya Lady JayDee jumapili hii saa tatu kamili EATV.

No comments:

Post a Comment