Friday, May 10, 2013

SHEIK PONDA NA USTAADH MUKADAM WATOA TAMKO KALI LEO

Wakizungumza kwenye msikiti wa mtambani Kinondoni mara baada ya swala, Sheikh ponda na ustaadh mukadam  wameapa kupambana hadi dakika ya mwisho. 
Mukadam amemsifia Allah kwa kuwapa adhabu ya ugonjwa,watu kadhaa akiwemo  mkubwa mmoja  alie mahututi Afrika kusini(wanadai  eti alihusika kuwatengenezea mashtaka),na afisa mwingne wa jeshi kufarik ajalini baada ya kuwanyanyasa selo!
KAULI ZA SHEIKH PONDA.
Alitamka  kuwa :"Nitapambana hadi mwisho' huku watu wakisema takbir alah akbar! Amesema Wakristo wanapendelewa na serikali. Serikali ilisema aliekojolea kuran ni mtoto,wakati yeye kawakuta watoto jela akiwemo wa miaka 10,aliyekwapua mkoba.,ila yule mkristo wa miaka 14 serikali ilisema mtoto na haikumchukulia hatua zozote! 
Pia kasema ana CD zikionyesha jinsi serikali inavyoua na kupanga kukandamiza uislamu. Kampongeza sana Zitto kabwe kwa mchango wake wa kutetea uislamu bungeni na kamponda yule aliepeleka cd alizoita za uchochezi bungeni! 

Karudia tuhuma za kuwa NECTA kuna udini na Waislamu wanafelishwa! Kasema serikali inapendelea na kuendeshwa na wakristo. Pia kuhusu bomu la Arusha kasema, wamekamatwa waarabu ,mbona hawajakamata wazungu? Anasema huo ni mpango wa kuonea waarabu na uislamu! 
Ponda  kasema wakristo hajawahi kuuawa na serikali,ila waislamu 2 ndo wanauawa! Mwembechai waliuawa, Pemba waliuawa.Anadai hata Pemba Waislamu waliuawa na serikali ikitumwa na Kanisa! Amehoji,mbona hatujawahi kusikia mchungaj au padri kauawa?kasema pemba kuna helcopter zilikua zinalipua majahazi ya waislamu(wakiwa baharini) wakati wanakimbilia Mombasa naTanga.! 


Pia kasema,nchi hii hakuna udini,ila kuna mapambano ya waislamu kudai haki zao na redio iman imefungiwa kuwaonea waislamu wasipate pakusemea



Credit:  JAMIIFORAM

No comments:

Post a Comment