Tuesday, May 14, 2013

UJUMBE WA LEO:‘VICHECHE’ WA BONGO UINGEREZA MMEJIDHALILISHA KWA DIAMOND!

LEO nazungumza nanyi baadhi ya wanawake wazuri wa Kibongo muishio Uingereza. Asanteni kwa kujitokeza kwenye shoo ya mtoto wa nyumbani, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Reading, Uingereza.
Najua mbali na ninyi wenye maskani hapo Reading wapo waliohudhuria shoo hiyo wakitokea miji mingine kama London. Mlipendeza, mkainjoi muziki mzuri wa Bongo Fleva kutoka nyumbani.
Shukrani nyingine ziwafikie kwa kuonesha kuunga mkono muziki huo ambao hivi karibuni umezua tafrani.
Najua mpo mliofika mkiwa wenyewe lakini wengine mliambatana na ama waume au wachumba zenu.
Mliacha kazi zenu ili tu kumshuhudia Diamond mliyekuwa mkimsubiria kwa shauku kubwa

.
Ukweli ni kwamba baadhi yenu mlionesha hisia za mapenzi kwa Diamond na kusababisha tafrani bila kujali waume, wachumba na wapenzi wenu.
Mlionesha aibu. Upo wewe uliyemshika Diamond mwili tu ukakimbilia kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa nawe umekidhi haja zako kwa kitendo hicho.
Upo wewe uliyeshindwa kujizuia na kumfuata Diamond jukwaani kisha ukamlazimisha ‘kudendeka’ naye na kusababisha watu kupigwa na butwaa.
Ukweli ni kwamba Diamond alijitahidi kukukwepa kwani ulikuwa umeshagusisha mdomo wako na wake kabla ya kujichomoa maungoni mwako.
Ukae ukijua kuwa tukio hilo ni kujidhalilisha wewe na warembo wengine mliokuwa nusu utupu kwa vinguo vyenu vya aibu.
Weka pembeni ninyi ni cha mtoto, kuna wewe uliyemganda ukilazimisha kulala naye kwenye hoteli aliyofikia, matokeo yake ulipomkosa ukaanza kumlazimisha densa wake ukalale naye.
Kingine cha ajabu, baadaye ukawa unadai ulilala na Diamond ukisifia kuwa umekidhi haja zako.
Matokeo yake ninyi wenyewe mkaanza kutupiana vijembe mkijiita vicheche kwa maana ya kukosa kujisitiri na kujifunua tabia za baadhi yenu mliopo ughaibuni.
Mtakubaliana na mimi kuwa shoo hiyo pia ilihudhuriwa na watu wa mataifa mengine hivyo waliwaona mnavyolitia aibu taifa letu kwa kujirahisisha kwa mwanaume.
Je, mnataka tuamini kuwa ndiyo tabia yenu huko Ughaibuni? Au mliingiwa na pepo wa ngono kwa Diamond?
Mmelijengea taifa picha mbaya kwa mataifa mengine ya Afrika kama Kenya, Uganda na Nigeria ambao nao walihudhuria onesho hilo. Mnahitaji kuomba msamaha kwa Watanzania ambao wamepata picha ile kwani skendo ya Wabongo kujiuza ughaibuni ina chembechembe za ukweli. For the love of game!
chanzo:globalpublishers

No comments:

Post a Comment