Thursday, May 16, 2013

UKAHABA WALIGUSA BUNGE, HUU NDO UAMUZI SERIKALI ULIOCHUKUA. SOMA HAPA


BIASHARA ya ukahaba imeligusa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani Jumanne iliyopita takribani dakika nane zilitumika kuijadili inavyoshamiri na namna ya kuitokomeza. 

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Kundi la Vijana Mkoa wa Arusha, Catherine Magige aliyeanzisha mjadala.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Kundi la Vijana Mkoa wa Arusha, Catherine Magige, ndiye aliyeanzisha mjadala asubuhi katika kipindi cha maswali na majibu, baada ya kumuuliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kuhusu mpango wa serikali kudhibiti ukahaba.
Magige aliuliza kuhusu fikra za serikali juu ya mpango wa kupeleka muswada bungeni, kuhusu uundwaji wa sheria ya kudhibiti ukahaba nchini.
Swali hilo la Magige, lilikwenda sambamba na maelezo kuwa biashara ya ukahaba inavyoshamiri, inazidi kusababisha mmomonyoko mkubwa wa maadili.
Alisema, biashara hiyo vilevile ni kichocheo cha kushamiri kwa maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi, kuongezeka kwa watoto wa mitaani na kukua kwa uhalifu kwa sababu kuna uporaji hufanyika kwa kuwatumia hao wanaojiuza.
Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki alisema serikali inajitahidi kuimaliza biashara ya ukahaba nchini.



Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Aliongeza kuwa serikali inatumia taasisi mbalimbali za kijamii kuielimisha jamii kuhusu athari za ukahaba.
Magige, aliuliza maswali mawili ya nyongeza, moja akitaka kutungwa kwa adhabu kali, maana zile zitolewazo sasa zimeonekana ni dhaifu, pili akataka takwimu ya kesi za ukahaba ambazo zimesharipotiwa mpaka sasa.
Akijibu maswali hayo, Kairuki alisema kuwa umuhimu wa kutoa adhabu kali ni mkubwa lakini akasema tatizo ni jamii, kwani imekuwa ikiyajua madanguro ya makahaba lakini watu hawatoi ushirikiano.
Kuhusu takwimu, Kairuki alisema kuwa mwaka jana, ndani ya Jiji la Dar es Salaam, kesi 22 ziliripotiwa Mahakama ya Jiji na watuhumiwa 123 walihukumiwa.
Wakati huohuo, baadhi ya machangu wameliambia Amani kuwa watakuwa wakitembea na tindikali kama nyenzo ya kujilinda wanapokuwa katika shughuli zao.

No comments:

Post a Comment