WASANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Ney wa Mitego pamoja na Chidi Benz ambao wanaonekana kuvuta hisia za mashabiki wao kutokana na kulumbana hadharani ambapo kila mmoja anajiona zaidi
Hatua hii imekuja baada ya kulumbana kwa muda mrefu na mwazo wa wiki hii, Chid aliandika katika mtandao wake wa kijamii 'Facebook' kwamba Ney wa Mitego kapokea kichapo alipokwenda kutoa shoo Mbagala Dar es Salaam
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam Ney wa Mitego alisema kuwa anashangazwa na msanii mwenzake kumzushia kutukanwa pamoja na kupigwa na baadhi ya mashabiki waliojitokeza katika shoo iliyofanyika Mbagara jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
Alisema si kweli kwamba alipigwa kwani alipokelewa vyema katika shoo hiyo na na ameweza kuwapagawisha mashabiki wake waliohudhuria katika tamasha hilo hali ambayo kwake inamuonyesha hali ya kukubalika na mashabiki
Aliweka wazi kuwa kinachomuumiza msanii mwenzake Chidi ni mistari ya maneno yake anayoimba yanayomtaja msanii kutoboa pua hali ambayo anahisi kudharilishwa, na maneno hayo ndiyo yanayopandisha 'mzuka' kwa mashabiki
"Hakujatokea ugomvi wowote ule zaidi ya mashabiki wangu kuonyesha kukubali kile nilichokifanya kwani nilivua tisheti na kuwatupia pamoja na mkanda hapo ndipo walipokuwa wanagombania kwa kuvitaka vitu hivyo lakini shoo ilikuwa poa na mashabiki walipokea nilichofanya mzuka ulizdi pale ninapoimba kuhusu Chidi kutoboa pua pamoja na kuvaa kipini " alisema Ney wa Mitego
Akizungumzia kuhusu maelewano yao alisema kuwa maelewano yake na msanii huyo Chidi hayamsaidi kitu chochote na kwake hayana manufaa kwani hayamuongezei chochote kwenye maswala ya kimuziki na kimaisha kiujumla
Kwa upande wake Chidi Benz alisema kuwa alichokiandika kupitia mtandao wa kijamii 'Facebook' ni kile kilichotoka katika mtandao mwingine hivyo haoni sababu ya kuendelea kukizungumzia wakati teyari kimeshaandikwa
Alisema kuwa maneno yanayoimbwa katika nyimbo ya msanii mwenzake hajawahi kuyasikia zaidi ya kuwambiwa na watu wakaribu yake hivyo hajui anamaanisha nini
Alisema kuwa hanampango wa kuyafwatiria hayo maneno na wala kumuuliza chochote kwani kusemwa ameanza kusemwa muda mrefu hivyo kwake maneno hayana tija yoyote zaidi ya kuendelea mbele kimuziki
"Siwezi kumuuliza kitu kwani kusemwa nimesemwa sana hivyo kazi yangu ni kukaza buti kisanii tu na si vinginevyo maana siwezi kumzuia kuzungumza" alisema Chiddi
Akizungumzia juu ya mahusiano yake baina ya msanii mwenzie alisema kuwa mahusiano hayo yapo tu ingawa hana nafasi ya kumuuliza chochote kile kuhusu mistari yake anayoitunga inayomuhusu yeye
Wakati huyo huyo inasemekana msanii huyo Chidi alichezea kichapo kutoka kwa msanii wa hip hop 'Kala Pina' mwisho wa wiki katika shoo iliyofanyika Maisha Club jijini Dar es Salaam
Akijibu swala hilo la kupigwa Chidi alisema kuwa hajapigwa na msanii huyo zaidi ya kusukumwa alipokuwa ameshika mic kwa ajili ya kuimba baada ya tatizo hilo kutokea akaamua kushuka na kuachana naye kwa sababu shoo haikuwa yake
"Mimi sijapigwa ila mshikaji alinisikuma tu nikaamua kuachana naye kwani shoo haikuwa yangu nikaamua kuondoka zangu sikutaka kualibu shoo ya washikaji zangu" alisema Chidi
No comments:
Post a Comment