Wednesday, May 8, 2013

MASHABIKI WA BOSTON WAMZOMEA RIHANA KWA KUCHELEWA KUPANDA JUKWAANI, SOMA STORI NA CHEKI VIDEO YA TUKIO ZIMA


Rihanna alikutana na hasira za mashabiki wa Boston baada ya kuchelewa kupanda jukwaani masaa matatu baada ya milango kufunguliwa, ambapo mashabiki hao walishindwa kuzizuia hasira zao na kumzomea kwa nguvu.

Kwa mujibu wa mtandano wa Boston.com RiRi alipanda kujwaani saa nne na nusu usiku wakati fans waliingia ukumbini saa moja na nusu, na kwamba alitarajiwa kupanda jukwaani angalau saa tatu kamili usiku.

Lakini pia msanii aliyetakiwa kufungua tamasha hilo A$AP Rocky alishindwa kupanda jukwaani kwa sababu alikuwa mgonjwa.

Gazeti moja la maarufu la udaku la Uingereza limeripoti kuwa Rihanna alikuwa anaangalia mechi ya mpira wa kikapu ya Chicago Bulls wakati fans wanapigwa dolo kumsubiri jukwaani.

Show hiyo ya Rihanna iliwahi kuahirishwa March 10 baada ya kuugua na sasa fans walikuwa wanaisubiri kwa takribani miezi miwili.

Baada ya show Rihanna alipost kwenye Instagram na twitter, “I will never forget this night!!! I truly have deeper love for you now!!! Thank you for making it extra.

No comments:

Post a Comment