Mwanamuziki Judith Wambura, amepigwa stop na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kinondoni kuongelea lolote kuhusiana na ugomvi wake na viongozi wa Clouds Media Group, nje ya mahakama mpaka hapo kesi yake ya msingi dhidi ya viongozi hao ambao ni wadau wa burudani itakapomalizika.
Katika status yake aliyoiandika muda mfupi tu kupitia ukurasa wake wa Facebook, Lady Jaydee ambaye siku za karibuni amekuwa maarufu kwa jina la Anaconda amesema:
"Nadhani baada ya hii, maswali yatapungua kama sio kuisha kabisa...Nafahamu kila mtu anasoma kwa wakati wake pengine hamkuona sababu nilizoelezea kwanini sijatoa waraka mwingine Tar 15 kama nilivyo ahidi.
Sababu ni kuwa mahakama imesema nisizungumzie hilo swala kwasasa, ambapo kesi bado iko mahakamani...Mpaka nitakapopewa ruhusa ya kuzungumza au kutozungumza tena".
-
Mdimuz
No comments:
Post a Comment