Thursday, May 16, 2013

MSIGWA AGOMA KUMUOMBA RADHI KINANA NA BADALA YAKE AMEMSHAURI AENDE MAHAKAMANI KAMA ANADHANI ALIONEWA


Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amemtaka  katibu mkuu  wa chama  cha mapinduzi (CCM) Bw  Kinana  kutosubiri muda  wa  siku  21 alizozitoa  kumfikisha mahakamani na kudai kuwa  yupo tayari  kwenda mahakamani hata kesho.

Mbunge Msigwa amesema kuwa katika  ukweli  hatakuwa   tayari kumwogopa mtu na kuwa siku  zote atasimama katika  ukweli katika  kupigania maslahi ya Taifa  hili.
Mbunge  Msigwa amesema  kuwa hatua ya katibu mkuu  wa CCM kukimbilia katika  vyombo  vya habari  kutishia  kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika  kupelekewa taarifa  ni  sawa na kumwogopa na  hivyo suala la Kinana kwenda Mahakamani  si  sawa ni  kumtishia nyau mtu mzima.
Msigwa  alisema  Chadema  ina  mawakili  waliojitosheleza na  kuwa hawatanyamaza kusema  ukweli kwa  kuogopa vitisho vyovyote .
 Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi  wa  jimbo hilo leo  jioni katika eneo la stendi kuu ya mabasi ya mikoani
 Umati mkubwa  wa  wananchi  wakimsikiliza mbunge  wao wa  jimbo la Iringa mjini
 Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini Mchungaji ,Msigwa akiwahutubia  wananchi  wa  jimbo la Iringa mjini

No comments:

Post a Comment