Mchongo wa Familia ya Amante kutaka kuhamia Dubai, ambako ndiko Amante alikuwa amepata kazi baada ya misuko suko mingi iliyoikumba familia yake na kujikuta akifilisika, ulipelekwa jela na Clara ambae alimwambia baba yake Gary aliyekuwa jela kuwa Alvira na familia yake wanataka kuhamia Dubai.
Gary kusikia hivyo kwakuwa anampenda Alvira, aliamua kupanga mbinu za kutoroka jela na kuibuka fasta uraiani.
Baada ya Gary kufanikiwa kutoroka jela, anamteka Alvira na kumficha pasipo julikana, huku akimlazimisha akubali kuwa anampenda yeye na sio mumewe Amante.
MARA na Christian wakiwa njiani katika harakati za kumtafuta Alvira, jambazi anatokea na gari moja dogo jeusi na kumshuti MARA,lakini anamkosa.
Kumbe Amante alikuwa mbele ya lile gari, naye alijibu mashambulizi ya risasi kwani naye amenunua bastola kutokana na maudhi ya Gary. Amante anafanikiwa kumteka jambazi na kumkabidhi kwa maaskari.
MARA anazidi kuwa na wasi wasi na Clara huenda akawa nahusika katika mkakati wa kumteka mama yake Alvira.
Anaamua kwenda nyumbani kwa akina Clara na kumuuliza ni kwanini yeye hajishughurishi katika kumtafuta mama yao? Clara anashindwa kujibu na kuamua kuanza kupigana, wakiwa wanapigana mama yao Suzan anawaachanisha.
Clara anaamua kwenda alikotekwa Alvira, na kujionyesha kuwa anahusika pia katika utekaji huo.
Alvira analia kwa uchungu akimuuliza Clara, nikwanini nayeye ameamua kumfanyia hivyo. Lakini Clara kwa ujasiri alijibu “wewe si ulinisaliti na kumchagua MARA kuwa ndiye unayempenda?”
Siku iliyofuata baada ya Clara kukwaruzana tena, mama yake Clara “Suzan” alimuamru MARA aondoke, MARA aliamua kuingia mtaani, akiwa anashangaa shangaa, mara akamuona Clara anakatiza mtaani.
MARA anaamua kumfuata Clara kwa nyuma nyuma hadi anafanikiwa kuingia alikofungiwa mama yake “Alvira”.
MARA anamnyanyua mama yake ili watoroke, lakini kabla ya kutoroka , alimpigia simu baba yake na kumuambia maeneo waliko.
Akiwa bado anaongea Gary na Clara waliingia na kuwanyang’anya simu na kuwafunga kamba. Kutokana na kila wakati Clara na MARA wanapokutana lazima wapigane, sasa Gary anaamua kumfungia MARA kabatini.
Muda mfupi polisi wanafika eneo hilo, Gary anajidai kumteka mwanae Clara kwa kumuwekea bastola kichwani, na endapo polisi wakijaribu kumsogelea, basi atamshoot.
Akiwa bado amemshikilia Clara mara risasi inapigwa. Je, ninani kapigwa? Gary au Clara? Na kama sio hivyo, Gary atamshoot Clara?
Itaendelea..
[Mwandishi Vikta Machota]
No comments:
Post a Comment