Friday, May 10, 2013

TFF imemtaka Mwandishi wa Clouds FM kutoa maelezo ndani ya siku saba


Mtangazaji wa Clouds Fm na mmiliki wa shaffihdauda.com akifuatilia jambo wakazi wa kazi zake
 MTANGAZAJI wa Clouds FM ambaye pia ni mmiliki wa tovuti ya www.shaffihdauda.com ameingia matatani baada ya kudaiwa kuweka nyaraka za siri za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwenye mtandao wake. TFF imemtaka Shafiih Dauda  kutoa maelezo kuhusiana na barua ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye mtandao wake huo huku akijua kwamba barua hiyo ilikuwa ni
siri.


Barua hiyo ambayo TFF walitumiwa na FIFA kuelezea hatua za kuchukuliwa kutokana  na kusimamishwa kwa mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamika, FIFA baadaye ilitoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa barua ambayo ilituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga.

Rais wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao Dauda alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila kuondoka nayo.

Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya siku saba.

source-habarimpya

No comments:

Post a Comment