Wednesday, May 15, 2013

LULU MWIGIZAJI MWENYE MVUTO MITANDAONI.


Elizabeth
 Michael
Lulu mkali wa filamu Swahiliwood.
UNAPOKUWA mtu maarufu unafuatiliwa kwa vitu mbalimbali, pengine unapokuja katika tasnia ya filamu ungependa kufahamu kuwa ni msanii gani mwenye mvuto katika mitandao ya kijamii ambaye tu anpofanya tukio lake na video hiyo ikawekwa katika mitandao ya kijamii na kufunguliwa na kuangaliwa na watu wengi.

Kwa utafiti uliofanywa na FC msanii mwenye mvuto katika mitandao na kufuatiliwa habari zake na watu wengi ni 

Elizabeth Michal ‘Lulu’ ambaye ndio msanii anayeongoza kwa video za matukio yake kuwa na mvuto na kutembelewa na watu wengi baada ya video yake tu kuwekwa katika mtandao kwa mujibu wa mtandao wa Youtube.

Kama ilivyo kwa wasanii wa nje ambao ujulikana kwa kuwa tofauti na watu wengine ambao si nyota ndio maana 
Ulimwengui sasa unamuongelea msanii wa Marekani Lady Gaga kama ndio msanii mwenye marafiki wengi katika akaunti yake ya facebook na kuwapita watu wote ambao ni wanachama wa mtandao huo kwa nyumbani kipimo chetu ni kupitia mitandao pia.

Wema Abraham Sepetu
Wema Sepetu msanii mwenye mvuto.
Steven Kanumba
Marehemu Kanumba mwigizaji nyota Swahiliwood.
Msanii Lulu ambaye ndio mwenye mvuto na wapenzi wengi katika mitandao ya kijamii amewatupa wasanii wenzake ambao ndio nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood katika mchakato huo Lulu kwa mwaka mmoja video zake zilizowekwa kupitia youtube zimetazamwa na watu zaidi 749,961 idadi ambayo haijafikiwa na msanii yoyote.
Katika kuonyesha kuwa msanii Lulu ni kipenzi cha watu ambao ufuatilia habari kupitia mitandao mbalimbali hivi karibuni alipotoka lupango na kufanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kutimiza miaka ya utu uzima yaani miaka kumi na nane video ya sherehe hiyo tayari imetazamwa na watu 58, 346 jambo ambalo linaonyesha kuwa ana mvuto kupitia mitandao.
.
Elizabeth Michael
Lulu akiwa katika pozi
Irene Uwoya
Irene Uwoya mwigizaji Swahiliwood.
Msanii mwingine ambaye pia video za mahojiano yake au matukio yake nje ya filamu anayefuatia kwa mbali baada ya nyota Lulu ni Wema Abraham Sepetu wengi hata mimi pia nilikuwa nafikiria anaweza kuwa na alama nyingi kumpita Lulu lakini hali ipo tofauti kwani yeye video zake zimetazamwa na watu 442,
874 kwa mwaka mmoja.
Nyota mwingine wa filamu ambaye mahojiano yake yametazamwa na watu wengi ni marehemu Steven Kanumba ambaye amejipatia alama nyuma ya msanii ambaye alimtoa kisanaa Wema Sepetu marehemu ana alama 434, 104 naye kwa takribani mwaka mmoja toka kuwekwa kwa Video zake kupitia mitandao ya kijamii.
Baada ya kuingia mwanamume anayefuatia kuwa kivutio cha wapenzi wa filamu kuangaliwa kazi zake kupitia mitandao ni mwanamke mlimbwende Irene Uwoya ambaye video yake imeweza kutazamwa na watu 367, 707 kama shindano tuseme anashika nafasi ya nne katika wasanii wanaovutia na kufuatiliawa na wapenzi wa filamu Bongo.
Msanii anayefuatia naye kuvuta watu wengi kuangaliwa ni marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ huyu ameweza kutazamwa na watu wengi kupitia mitandao kwa miezi saba tu baada ya video zake kuwekwa katika mitandao ya kijamii na kupitiwa na watu 130, 754 katika wasanii wa filamu huyu ndio anayefunga namba kwa wasanii wenye mvuto kupitia mitandao ya Video.
Hali inashangaza kwa wasanii ambao inaonekana kuwa ndio vinara wa mauzo ya filamu lakini video zao zimetazamwa na watu wachache sana baada ya kuwekwa na katika mitandao ya kijamii kwa kukosa watazamaji kwa idadi kuwa ya watazamaji, jibu lake ni rahisi tu wasanii hawa wameathiriwa kwa kukosa ukaribu na vyombo vya habari hasa Televisheni.
Amri Athuman
King Majuto mkali wa Komedi Bongo.
Wasanii waliothiwa na hali hiyo ni Ray ambaye kupitia mtandao wa you tube yeye mahojiano yake yamepatika katika akaunti moja tu ya Youtube Mkasi video yake imetazamwa na watu 59, 211 tu, na hakuna sehemu yoyote ambayo ungeweza kupata mahojiano ya msanii huyo mwenye jina kubwa Swahiliwood huku akiwa ni mwenye nafasi katika magazeti kuandikwa sana.
Wengine ni Jaqueline Wolper naye video yake inapatikana sehemu moja tu na video yake kutazamwa na watu 50, 582 tu, Monalisa ambaye video yake imetazamwa na watu 33, 500, akifuatiwa na Muhogo Mchungu mwenye watu 30, 359, huku hali ikiwa mbaya sana kwa Aunt Ezekiel ambaye Video yake zaidi miaka miwili imetazamwa na watu 23, 616 tu.
Jacob Stephen
JB mwigizaji asitambuliwa na mitandao ya kijamii.
Wakati wasanii wengine ni agharabu habari kupata habari kupitia mitandao ya kijamii kama vile msanii mkubwa kama Jacob Stephen ‘JB’ msanii huyo hana taarifa yoyote iliyopandishwa na kutazamwa na mtu, utafiti unaonyesha kuwa msanii kama JB si mpenzi au hajui umuhimu wa kuongea na vyombo vya habari jambo ambalo linamfanya kufanya mahojiano kwa njia ya simu tu na watu kukosa takwimu kupitia mitandao ya kijamii.
Elizabeth Michael
Lulu nyota ing'arayo mitandaoni.

Msanii ambaye baada ya mwaka mmoja inawezekana ndio akawa kinara wa habari zake kusomwa na kutazamwa na watu wengi ni King Majuto ambaye video yake ya mahojiano imewekwa kwa wiki mbili tu na kutazamwa na watu 31, 463 huku kazi zake alizoigiza zikiwa zimetazamwa watu zaidi 674, 461kwa baadhi ya komedi.
Huu ndio utofauti wetu sisi wa kawaida na nyota pia ikumbukwe kuwa alama zilizotajwa ni Video zilizohusu mahojiano tu na si matangazo au filamu za zilizowashirikisha wasanii hao, katika mchakato huo akinadada ndio wameshika chati kwa kazi zao kuangaliwa katika mitandao ya kijamii.

No comments:

Post a Comment