Friday, May 10, 2013

"CHIDIBENZI NI MDOGO WANGU NA UNGA ANAOVUTA UNAMPELEKA PABAYA NDIO MAANA NIKAMPA KICHAPO"-KALAPINA


                                        Kalapina kulia akiwa na fan wake
Baada ya muasisi wa harakati za hip hop Tanzania Kalapina kumchapa Rapper Chidi Benz katika jukwaa la maisha club alfajiri , Kalapina ameelezea sababu za kutoa dozi hiyo kwa msanii mwenzake, namnukuu " ukweli ni mambo fedheha, mdogo wetu chidi benzi cocaine au heroin / unga anaovuta unampeleka pabaya, tena mimi kama kaka yake namshauri aachane na matumizi ya madawa kulevya, kwa sababu mwisho wake utakua m'baya, mimi nilikua back stage na ikafika zamu yangu kupanda jukwaani nikawa naskia sauti mtu anatamba jukwaani kwa dakika saba ama nane, alikua ananichelewesha kupanda, na ananiharibia show yangu, huyu mtu si adui, nikatoa amri mara tatu kama F.F.U aka kaidi ndipo nikamfata na kumpa dozi, siku akaanguka chini na mimi nikaendelea na show yangu, hakuna hata mtu mmoja atakaye kubali kuharibiwa kazi, hata rais Kikwete ukimharibia utaishia jela."

No comments:

Post a Comment