Saturday, May 11, 2013

Kwanini Tanzania inang'ang'nia kwenda Kupigana Congo (DRC)?



Kuna mambo mawili yanaleta tafakari isiyo na ulinganifu japokuwa yaweza kuwa na mwelekeo unaofanana, ila kiuhalisia unakinzana.

Mosi, baada ya kutangazwa rasmi kuwa Tanzania itapeleka majeshi yake Congo, waasi wa M23 wameitaka Tanzania isipeleke jeshi lake huko. Kwanini M23 wanapinga sana Tanzania kuleka jeshi lake huko? Kwanini kelele zao ni kubwa sana kwa Tanzania lakini wako kimya kwa mataifa mengine? Je! Ni kwamba wanaiogopa Tanzania ama wanaionea huruma Tanzania, kuna nini kati ya nchi hizi mbili?

Pili, pamoja na kukatazwa kwenda Congo na M23, kwanini Tanzania tunang'ang'ania kupeleka jeshi huko? Pamoja na hali ngumu ya kiuchumi tuliyonayo watanzania kwanini Nshodha na Membe wanasisitiza jeshi letu kwenda huko? Ok, mtu aweza kusema kwasababu Rais alikubali kupeleka jeshi. Je kwanini Rais akubali kirahisi kupeleka jeshi Congo wakati suala kulitoa jeshi nje ya mipaka yako ni suala lenye kuhitaji tafakari kubwa zaidi?

No comments:

Post a Comment