Friday, May 10, 2013

MAMA DIAMOND, PENNY WAFANYA SHEREHE


  Na Erick Evarist
 WAKATI nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa Uingereza kwa ziara ya kimuziki, mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ na mkwewe mtarajiwa, Penny wameangusha bonge la sherehe katika Hoteli ya Serena, Posta jijini Dar.
Habari za kuaminika zilizotua kwa paparazi wetu zilidai kwamba, Jumamosi iliyopita Penny ambaye ni DJ wa Runinga ya DTV alikuwa akitimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa hivyo akawa amejipanga kufanya sherehe yake ndogo ya kuzaliwa huku mama wa msanii huyo akiwa naye amejipanga na dada yake Diamond, Esma ‘Kardashian’ kumfanyia sherehe mtangazaji huyo.
 
Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina kilidia kuwa, Penny alipania kweli kufanya sherehe hiyo na ubavu wake Diamond lakini mambo yakawa ndivyo sivyo baada ya jamaa kupata shoo hiyo pande za Uingereza.


“Penny ametimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa sasa alipenda kufanya pati hiyo na Diamond sema bahati mbaya jamaa yupo Uingereza kwa hiyo akaamua kufanya na familia ya staa huyo ili kujiliwaza,” kilisema chanzo makini na kuongeza:
“Penny alijiandaa kwa upande wake, mama Diamond naye na dada Esma wakajiandaa hivyo wakaungana pamoja na kuangusha bonge la sherehe lililohudhuriwa na watu mbalimbali baadhi yao wakiwa ni mastaa.


 
Picha ambazo Ijumaa imezinasa zinaonesha pati hiyo ilifana kwa misosi, vinyaji vya kufa mtu ambapo wageni waalikwa walikula hadi kusaza na kila mmoja aliwapongeza waandaaji wa sherehe hiyo ambayo waliifananisha na send off.
 
Imeelezwa kuwa, baada ya kumalizika kwa sherehe hiyo Diamond alimtumia Penny salamu za pongezi akiwa Uingereza na kumuahidi kumletea bonge la zawadi pindi atakaporejea Bongo.
Mbali na ndugu, jamaa na marafiki wa mastaa hao kuhudhuria, mastaa mbalimbali wa filamu na muziki walitokea kumuunga mkono akiwemo Mtangazaji wa Televisheni ya Star TV, Sauda Mwilima na Rommy Jonson ambaye ni kaka’ke na Diamond.

No comments:

Post a Comment