Thursday, May 9, 2013

PETER OKOYE WA P-SQUARE AMETELEKEZA MAMA NA MTOTO...


Peter Okoye

Sakata kuhusiana na moja ya mabrothas wanaounda kundi la P Square, Peter Okoye kutelekeza mtoto huko London sasa limechukua sura mpya hasa baada ya kufahamika kuwa, Mwanadada Elshamah Igbanoi ambaye ndiye mama mtoto aliyetelekezwa, ni kweli alikuwa na historia ya ukaribu na Peter kipindi cha nyuma.
Elshamah ambaye ana umri wa miaka 19 kwa sasa, ametuhumiwa kuwa amekuwa akimsonga msanii huyu kutokana na umaarufu wake, pia imethibitika kuwa ni binti wa kishua na ni kweli kuwa alikuwa na uhusiano na msanii huyu tangu akiwa na umri wa miaka 17.
Gonga continue reading kuendelea..

Peter alitoa ahadi mapema ya kwenda London kwa ajili ya kupima DNA kudhibitisha uhusika wake kwa mtoto aliyezaliwa lakini mpaka sasa bado hajafanya hivyo, na kwa upande wa Elshama, yeye pamoja na mtoto wanaendelea poa kwa sasa na mtoto tayari amepewa jina Mishel Paul Okoye.

No comments:

Post a Comment